Jiongeze: Kidume ishi namna hii….

Jiongeze: Kidume ishi namna hii….

Usiishi kikondoo bro. Jiunge walau na mtandao mmoja wa kijamii. ‘Kipu in tachi’ na washikaji. Kuna wana toka praymari hamjaonana, utawakuta mitandaoni.

Unaweza kupata mchongo au kujifunza ishu mbili tatu, au kuwa mzinguaji zaidi ukiamua.
Maisha mafupi sana, jitahidi kupunguza kukunja ndita. Jiachie mara moja moja.

Ukiwa baa msifie mhudumu kabla hujaagiza tungi. Ukimsifia baada ya fundo kadhaa za biere hata wao hupuuza wateja wa aina hii.

Na ukifika baa uwe tayari unajua unakunywa nini na cha baridi au moto.
Siyo mhudumu anakuja kukusikiliza unaanza kuwaza na kujiuliza unywe nini.
Inaonesha hujisomi na huna mipango yoyote mjini. Samahani lakini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags