Justin Bieber avunja rekodi

Justin Bieber avunja rekodi

Huko mitandaoni unaambiwa kuwa msanii kutokea nchini Marekani, Justin Bieber amevunja rekodi ya muda wote iliyokuwa ikishikiliwa na msanii Ariana Grande katika mtandao wa Spotify na sasa anakuwa ndiye msanii kinara anayesikilizwa zaidi.

Bieber amefanikiwa kufikisha idadi ya wasikilizaji Milioni 83.3 kwa mwezi na kumfanya ashike nafasi ya kwanza katika mtandao huo maarufu.

Hapo awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Ariana aliyekuwa na jumla ya wasikilizaji Milioni 823 kwa mwezi.

Najua msomaji wetu zipo ngoma unazozikubali za Bieber je tuambie ni ipi, dondosha coment yako katika ukurasa wetu wa Instagram wa @mwananchiscoop.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags