Kai ashikiliwa na polisi kwa kugawa playstation

Kai ashikiliwa na polisi kwa kugawa playstation

Mtayarishaji wa maudhui aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia  mitandao ya kijamii kama #TikTok, #Instagram, #YouTube pamoja na #Twitch kutoka Marekani Kai Cenat, ameshikiliwa na ‘polisi’ kwa tuhuma za kuchochea ghasia na mkusanyiko wa watu kinyume cha sheria Manhattan.

Matukio hayo yametokea baada ya Kai kutangaza kupitia kurasa  zake za mitandao yake ya kijamii kuwa atagawa bure Playstation 5, kwenye mtaa wa  Union Square Park mjini New York.

Mamia ya vijana walifurika mapema kwenye mitaa hiyo kwa ajili ya kupata Playstation za bure na kupelekea baadhi yao kuwafanyia fujo ‘polisi’ waliyokuwa wakiwatawanyisha eneo hilo.

Kulingana na taarifa ya Idara ya polisi ya New York (NYPD), inaeleza kuwa takribani watu 65 walikamatwa katika ghasia hizo, wakiwemo watoto 30.

Kwa upande wa Kai naye anashikiliwa na polisi kwa sababu hakuwa na kibali cha kuandaa mkusanyiko huo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags