Kambi za wakimbizi zaathirika na utapiamlo

Kambi za wakimbizi zaathirika na utapiamlo

Shirika moja la kutetea haki za binadamu limeelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa utapiamlo kwenye kambi za wakimbizi kasakazini mwa nchi ya Kenya.

Moja ya chombo cha habari kimeeleza kuwa watoto wameathirika zaidi, wakati viwango vya chakula vikishuka kutokana na kupungua kwa misaada.

Idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini kutokana na utapiamlo imeongezeka kwa karibu asilimia 95 mwezi Mei, ikilinganishwa na mwezi uliopia kwenye kambi ya wakimbizi ya Hagadera.

Licha ya kuwa Kenya inatoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi 600,000, kwenye kambi za Daadab na Kakuma, pamoja na kwenye miji midogo.

Hali hiyo imetokea kwa ukanda Afrika Mashariki kukumbwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kufuatia kukosekana kwa mvua kwa misimu sita mfululizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags