Kamera ilivyobadili maisha ya Rosah

Kamera ilivyobadili maisha ya Rosah

Safari moja huanzisha nyingine msemo huu unajionesha kwa mwanadada Rosamaria Mrutu ambaye alianza kufanya kazi kama mwanahabari lakini baadaye akajikuta anaangukia kwenye u-videographer na photographer.

Rosa ambaye kwa sasa anafanya kazi Clouds Media ameiambia Mwananchi Scoop kuwa kazi hiyo ya kushika camera kwake ilikuja kama zali la mentali

"Sikuwahi kuwaza au kuota kama nitakuja kuwa mpiga picha, hii ilinikuta nikiwa tayari kwenye media industry nikiwa nimepita kwenye media kama tano kama mtangazaji wa vipindi vya burudani na producer wa vipindi. Clouds niliingia kama mtangazaji lakini baada ya muda nikaenda kusoma short course ya Video Shooting and Editing nikawa na-shoot kipindi.

"Clouds kuna mtindo wa baada ya muda vipindi kusimama ili kuboreshwa zaidi  kwa hiyo kwenye kile kipindi mimi nikawa sina kazi kiongozi wa Digital akaniuliza naweza kufanya nini nikamwambia ku-edit video,"amesema

Anasema ili kuwa mzuri zaidi kwenye upande huo wa kushika kamera na ku-edit boss wake alimkabidhi kwa walimu wa tatu kwa ajili ya kumnoa

 

"Siku moja akaja ofisini akaniambia kuanzia leo anataka niwe mpiga picha akamalizia kwa kuniambia nisimuangushe akanipatia walimu watatu mmoja anaitwa Dalidali ndiye mtu wa kwanza kunifundisha kupiga picha wa pili anaitwa Mwakajana akawa mwalimu wangu mzuri zaidi, wa tatu akawa Octa Nyox kwa ajili ya kurusha vipindi vya redio Youtube live nikawa mpiga picha mzuri na nikaweza kurusha matukio live ninajivunia hilo,"amesema

 

Licha ya kuwa kupitia shughuli ya u-videographer na photographer zimekuwa zikimpatia mafanikio mengi anasema awali ndoto yake ilikuwa awe mwanamitindo 

"Ndoto yangu tangu utotoni ilikuwa haihusiani na chochote ambacho kinahusiana na masomo ya darasani nilikuwa napenda urembo, kuimba na kudansi katika ukuaji wangu wote nilijua nitakuja kuwa mwanamitindo mkubwa lakini bado naishi kwenye fashion,"amesema

 

Hata hivyo amesema mwamko wa watu kwenye kuthamini kazi ya upigani picha bado mdogo

"Watu wengi wanachukulia mpiga picha kama kitu kidogo anachukuliwa poa kuna muda unatoa gharama ila mteja anaona ni gaharama kubwa hajui unapitia procedure gani hadi kitu anachotaka apate, kingine inaonekana kama roboti watu wakiwa wanakula wewe hutakiwi kula unatakiwa kupiga picha kuna sehemu watu wanalia au wanaomba wewe unatakiwa tu kupiga picha. Ingawa kwangu imekuwa tofauti kidogo kwa sababu nimefunguliwa milango mingi ya baraka nimekuwa nikipata nafasi ya kukaa na wakuu,"amesema

 

Amesema ili idadi ya wanawake wanaofanya kazi kama yake iongezeke basi inahitajika wenyewe kwanza kujiamini na watoaji wafursa wawapatie bila kuwafanyia unyanyasaji wa kingono.

"Kwanza mwanamke kujiamini angalia kesho yako na maisha ya sasa yanataka nini Mungu anakusudi kukuumba mwanamke na tuna akili nyingi kuliko wanaume jaribu kuangalia kitu atachopatiwa mtoto wa kike kufanya hata kama kinaaminika cha kiume basi atafanya kwa uhakika tusichague kazi ukipata kazi fanya, mtangulize Mungu, jitihada na imani kisha pambana usiangalie nani anasema nini kuhusu wewe,"amesema

Kupitia kazi hiyo anayofanya imempatia mafanikio kama vile kuwa na usafiri wake, kuendesha maisha yake na hata kumsomesha mwanaye 

Rosa hakuacha kutoa shukran kwa waliomshika mkono, "bila Mecky Kaloka nisingeingia kwenye Camera Operating yeye ndiye amenifungulia njia bila rushwa ya ngono ana nafasi kubwa kwenye maisha yangu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags