Kampeni ya ukusanyaji damu kufungwa Septemba 25 kwa kishindo

Kampeni ya ukusanyaji damu kufungwa Septemba 25 kwa kishindo

Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro imepanga kufunga kampeni yake ya ukusanyaji damu salama Jumamosi Septemba 25 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala, Amana.

Katika ufungaji wa kampeni hizo, kutakaohusisha pia huduma za kuwasaidia wagonjwa na kusafisha maeneo ya hospitali hiyo sambamba na huduma za utoaji damu kwa hiari.

Akizungumzia ufungaji wa kampeni hiyo iliyozinduliwa Septemba 20 mkoani Morogoro, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mpango wa Damu Salama, Dk. Pendalieli Joseph amesema timu ya watoa huduma kutoka vikundi 15 vitashiriki ili kutoa huduma kwa watoa damu.

Naye Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk. Avelina Mgasa amesema kauli mbiu ya kampeni za mwaka huu ni ‘Changia Damu Kuokoa Wanaoleta Uhai Duniani’.

Dk. Mgasa amesema kampeni inayoendelea ni ya robo ya mwaka 2021 hadi 2022 yenye lengo la kukusanya chupa 19,514 nchi nzima zitakazokusanywa na timu za kukusanya damu 226.

Kanda nyingine za Mpango wa Taifa wa Damu Salama ni Kanda ya Ziwa inayohudumia mikoa ya Mweanza, Simiyu, Geita, Mara, Kagare na Shinyanga na Kanda ya Magharibi kwa mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, na Singida.

Nyingine ni Kanda ya Kusini inayohudumia mikoa ya Lindi na Mtwara; Kanda ya Kaskazini inayohudumia mikoa ya Kilimanyaro, Tanga, Arusha na Manyara  pamoja na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayohudumia mikoa ya Mbeya, songwe, Njombe, Rvuma na Iringa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags