Kayumba adai kudhulumiwa 1.8 milioni

Kayumba adai kudhulumiwa 1.8 milioni

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Kayumba Juma ameweka wazi juu ya mwendelezo wa sakata lake alilodai awali kudhulumiwa Sh 7 milioni na Director Elly Mzava, ambaye anafanya kazi na Rayvanny chini ya lebo ya Next Level Music.

Kayumba amesema kiasi hicho cha pesa alikilipa kwa ajili ya kufanya wimbo wake wa ‘Shake’ na Rayvanny 'Chui', lakini hakufanikiwa na pesa imechukuliwa.

Wimbo huo ambao upo katika album yake ya ‘Fine Tape’ ambapo video yake inadaiwa ilikuwa inatarajiwa kutengenezwa mwaka 2023 lakini mpaka sasa haijatengenezwa kutokana na sakata hilo.

Febuari 21, mwaka huu Kayumba aliweka wazi chati za maongezi na uongozi wa Next Level Music zilizoonesha anaomba pesa yake irudi na kulalamika kuwa amefanyiwa utapeli.

Mbali ya kuweka wazi mawasiliano na kuomba Serikali imsaidie amesema hadi sasa   anadai 1,800,000 milioni, akiwa amelipwa 5200,000 milioni tu.

Akizungumzia suala hilo Kayumba ameiambia Mwananchi kuwa hata baada ya kuliweka mitandaoni jambo hilo bado wadeni wake hawakupokea simu.

"Kwanza baada ya kufunguka mtandaoni niliitwa na Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma kwa ajili ya kutafuta namna ya wao kunipa pesa zangu, tuliwapigia simu lakini hawakupokea, basi kiongozi aliniambia mimi nitulie yeye atalifuatilia hilo suala, hadi leo wapo kimya,” amesema.

Aidha ameongezea kuwa kwa sasa Director Mzava na Rayvanny hawafanyi naye kazi kama zamani tangu alipoamua kuwaweka hadharani, hivyo kila mtu amejenga chuki hakuna mazoea kama ya mwanzo.

Alipotafutwa Director Mzava kujibu tuhuma hizo hakutaka kuzungumzia suala hilo na kujibu kwa ufupi.“Kama ni mambo mengine niulize, lakini kwenye suala hilohilo subiri nitakupigia,” amesema na kakata simu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags