KIFAHAMU KIKOSI CHA WALINZI WA KIKE KILICHOKUWA KIKIMLINDA GADDAFI

KIFAHAMU KIKOSI CHA WALINZI WA KIKE KILICHOKUWA KIKIMLINDA GADDAFI

Tangu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi mikononi mwa kundi la waasi mnamo Oktoba 2011 mengi yameandikwa na kusemwa juu yake.

Lakini hakuna mengi yaliyosemwa kuhusu kikosi cha walinzi wa kike ambao walikuwa wakiandamana naye kote katika safari zake.

Alijulikana kwa kuwapenda wanawake na kiongozi huyo wa zamani wa Libya alioa mara mbili. Alikuwa na wake wawili, binti na mamia ya walinzi wa kike waliokuwa wakijihami vikali kwa bunduki. Kulikuwa pia na muuguzi wa Kiukreni na wafuasi wengi wanawake ambao walisimama karibu naye wakati wa maisha yake.

Mkewe wa kwanza alikuwa mwalimu wa shule. Walitengana baada ya miezi sita na wana mtoto wa kiume - Muhammad. Mkewe wa pili, Safia al-Gaddafi, muuguzi kwa taaluma, ndiye mama wa wanawe wengine saba.

Walakini, kati ya wanawake wote maishani mwake, wale maarufu zaidi, labda, walioonyeshwa naye walikuwa walinzi wake wa kike waliozungumziwa sana. Jeshi lake la walinzi wanawake na timu za wauguzi wa kike zilimpatia umaarufu ulimwenguni.

Kulingana na ripoti, walinzi wake, pamoja na kuwa wanawake, walichaguliwa kwa kuwa mabikira. Kwa kuongezea, walipaswa kuchukua kiapo cha usafi na kuapa kuyatoa maisha yao kwa ajili yake. Inavyoonekana, walichukua viapo vyao kwa uzito - inasemekana hakuenda mbali naye mchana au usiku.

 

Walinzi hawa waliofunzwa walikuwa na ujuzi wa kijeshi na walikuwa wataalam katika utumiaji wa silaha, kulingana na ripoti mbalimbali za habari nje na ndani ya Libya. Jarida la Huffington lilisema wanawake hao walipata mafunzo mengi ya kijeshi na silaha katika chuo kikuu maalum kabla ya kuingizwa rasmi.

Gaddafi lazima alifikiri ilikuwa na maana kufundisha wanawake wazuri na kuwageuza kuwa wauaji. Wakiwa wamejipamba kuvutia na kuvalia viatu virefu katika nchi ambayo wanawake walivalia mavazi ya kiislamu hakika ni jambo ambalo liligeuza vichwa vya watu wengi

Jinsi Bin Laden, Saddam na Gaddafi walivyosakwa na kukamatwa au kuuawa.

Walinzi wa Gaddafi walikuwa sawa na utawala wake. Angewatumia kama ishara ya imani yake katika ukombozi wa wanawake. Hata hivyo baadaye ufichuzi wa kutisha ulitolewa na baadhi ya wanawake waliokuwa katika kikosi hicho kwamba Gaddafi alikuwa akiwabaka na kuwafanyia unyanyasaji mwingine.

Ziara ya Gaddafi nchini Italia mnamo 2009 iligonga vichwa vya habari baada ya kutolewa mwaliko wa wasichana 500 wa kuvutia wa Italia kwa dhifa ya chakula cha jioni katika jumba ambamo Gaddafi alikuwa akilala.

Inasemekana alitumia hafla hiyo kuwashawishi wasichana hao wasilimu na akawapatia nakala ya kitabu chake cha Green Book.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post