Kipande cha mlango kilichookoa maisha ya Rose wa Titanic chauzwa

Kipande cha mlango kilichookoa maisha ya Rose wa Titanic chauzwa

Kipande cha mlango wa mbao kilichookoa maisha ya Rose wa filamu ya Titanic kimeuzwa kwa dola 718,750 ikiwa ni zaidi ya tsh 1.8 bilioni.

Kipande hicho kimeripotiwa kuuzwa katika mnada wa vifaa na mavazi wa Heritage Auctions Hollywood huku wauzaji hao wakiweka wazi kuwa kipande hicho kilicho tumika kwenye filamu hiyo ni cha mabaki yaliookolewa kutoka kwenye ajali ya Titanic mwaka 1912.

Vifaa vingine vilivyouzwa katika mnada huo ni pamoja na mjeledi kutoka Indiana Jones na Temple of Doom, ambayo iliuzwa kwa $525,000, Suti ya Spiderman inayovaliwa na Toby Maguire iliuzwa kwa $125,000 na bidhaa nyingine.

Filamu ya Titanic ilitoka rasmi Disemba 19, 1997, ikioongizwa na James Cameron ambapo ilitumia bajeti ya dola 200 milioni na kufanikiwa kuuzwa na kupata faida ya zaidi ya dola 2.264 bilioni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags