Kiredio tishio mtaani mahusiano ya watu

Kiredio tishio mtaani mahusiano ya watu

Isaaaa Furahii dei yooh,  ni siku ya sisi kukutana na kufurahi pamoja kutokana na burudani ambazo tunazipata kwenye segment hii kupitia jarida letu pendwa la Mwananchi Scoop.

Code ni zilezile ili uweze kuifanya weekend yako iwe poa basi ni lazima upite kwanza kwenye magazine hii ili ufahamu tupo na nani kwenye burudani.
Week hii tupo na Vicent Njau ambaye watu wanamfahamu kwa jila la Kiredio, na wengi wakisikia jina hilpo au kumuona huyu jamaa basi wanatamani kupima hali ya mahusiani yao, kupitia Mwananchi Scoop Vicent anatusanua kwa nini anajiita Kiredio.

“Nilijiita Kiredio kwa sababu ni jina ambalo nimepewa  nikiwa darasa la tatu nilipewa na mwalimu wangu kama jina la utani, nilikuwa naongea sana alafu nilikuwa na mwili mdogo, wanafunzi wakacheka wakaanza kunitania mpaka nafika darasa la tano jina langu halisi likawa limepotea , ukiuliza Vicent  Njau hunipati ila ukisema kiredio watu wanasema kumbe huyo”. Anasema Kiredio

Licha ya kuwa na  elimu ya kutosha  Kiredio aliamua kuwekeza nguvu zake kwenye uchekeshaji tangu mwaka 2019, bila ya kufahamu kuwa mwaka 2023 jina lake litakuwa zaidi na kupendwa kutokana na anachofanya hasa baada ya kuanza kufanya maudhui ya kuwahoji watu kuhusiana na mahusiano yao.

“Idea ya content ninazotengeneza  zimekuja baada ya kugundua kuwa watanzania ni wambea sana, kwa hiyo nikaona tunafanya nini ili  waweze kufatilia kitu cha kimbea, nikajaribu kufanya na mtu anipe namba za mpenzi wake nimpigia alafu amtaje, idea ikaja hiyo nikafanya clip ya kwanza ikaenda mbali basi nikasema nishikilie hapahapa”. Anasema Kiredio

Miyeyusho ya hapa na pale kama kawaida inamkuta Kiredio hasa kutokana na kazi zake zinavyozidi kwenda mjini na watu kumfahamu zaidi amejikuta anapata ugumu wa kuandaa content anasema,

“Changamoto kubwa ni upatikanaji wa  content maana  nimeanza ku-straggle kwa sababu mwanzo video zangu zilikuwa hazijaenda kiukubwa  lakini sasa hivi wengi wananijua  sasa hivi nikimsimamisha mtu  wananikataa wanasema hawataki kuaibika, sasa hivi napata content kwa shida sana”. Anasema Kiredio

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakivutiwa na aina ya maudhui anayozalisha japo wapo wenye kutilia mashaka juu ya wahusika kwenye video zake kwa kudai kuwa huenda amekuwa anawapanga watu ili apate maudhui yakuvutia zaidi.

Kama ilivyotokea kwenye video iliyo-trend kwenye mitandao ya kijamii kuhusu msichana aliyekosa gari kwa kushindwa kutaja jina la mpenzi wake, ambalo kwa upande wa Kiredio ndilo tukio lililomfanya afahamike zaidi maeneo mbalimbali.

“Sijawahi kumpanga mwanachuo yeyote kufanya na mimi content ila wanachuo ndiyo kila mtu anatamani kujua status relationship ya mahusiano yake  kama anapendwa, kwa hiyo wananitafuta wenyewe,  kwa hiyo watu wakiona naenda kumpokea mtu wanajua nimempanga lakini siyo kweli sijawahi kumpanga mtu”. Anasema Kiredio

Pamoja na changamoto anazokutana nazo kwenye kazi yake lakini ameweza kupata mafanikio kwani kwa sasa ni tofauti na mwanzo wa mwaka, sasa amekuwa na uwezo wa kulipia mahitaji yake muhimu na si hivyo tu amedai kuwa alikuwa mwanzo akimtegemea mama yake lakini kwa sasa anauwezo wa kumsaidia mama yake.

Hata hivyo content nyingi za Kiredio watu wamekuwa wakizipata kupitia mtandao wa TikTok, lakini mwezi Oktoba baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walifutiwa akaunti zao na Kiredio akiwa ni mmoja wao hapa anatueleza,

“Kufutwa kwa akaunti za TikTok hakukunirudisha nyuma kwa sababu, zaidi pamenipiga teke nimesogea mbele, TikTok ukifanya kazi nzuri unaweza kupata followers milioni moja kwa mwezi , kwa hiyo akaunti yangu mpya ndani ya siku sita walini-follow zaidi ya watu laki sita, kwa hiyo hakukunirudisha nyuma labda siku ikifutwa ya Instagram ndiyo nitachanganyikiwa”. Anasema Kiredio.

Aidha kupitia mtandao huo, waandaaji maudhui nchini wamezidi kuwa wengi na hutumia vipaji vyao kujipatia kipati, Kiredio ameileza Mwananchi Scoop namna ambavyo content creator wanachukuliwa nchini.

 “Content creators bado hatujapewa heshima kama wasanii wengine, kinachotakiwa kifanyike serikali yetu ianzishe tuzo kama ilivyo kwa muziki na filamu, waweke content creator wa kike na wa kiume, mwenye uandishi bora yaani vipengele kama ilivyo kwa wasanii.

Serikali yetu ‘ikitusapoti’ hapo hata tukivuka mipaka tukiwaambia watu tuna tuzo kutoka nchini kwetu tunazidi kupewa kazi na kuwa wakubwa”. Anasema Kiredio

Hata hivyo Kiredio ametoa ushauri kwa vijana hasa katika kufanya kazi na kuondokana na visingizio vya ukosefu wa ajira,

“Vijana tufanye kazi, na kutokukata tamaa mimi nimeanza kufanya ninacho kifanya 2019 nimekuja kuonekana na watanzania 2023 kwa hiyo ukiangalia miaka minne nyuma nilikuwa sina pakulala, nilikuwa nalala njaa, sina bando sina vocha lakini sikukata tamaa, pengine ningekata tamaa ningekuwa nalima kahawa huko Kilimanjara, kijana pambana hakuna kukata tamaa”. Anasema Kiredio

Tukutana next week endelea kutufatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii kwa jina la mwananchi scoop






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post