Baada ya kuwepo kwa majadiriano mbalimbali katika miatandao ya kijamii kuhusiano na kolabo ya mwanamuziki kutoka Kenya, Willy Paul pamoja na msanii wa Tanzania Phina, na sasa kolabo ya wawili hao tayari imeshatoka.
Utakumbuka siku chache zilizopita kulikuwa na mizozo kupitia mitandazo ya kijamii baada ya wawili hao kutangaza kuja na kolabo huku baadhi ya mashabiki kutoka Tanzania wakionesha kutopendezwa na kolabo hiyo baada ya Willy Paul kudhihaki wasanii wa Bongo Fleva.
Aidha kufuatia na sakata hilo Willy kupitia ukurasa wake wa Instagram alijibu tuhuma hizo akiweka wazi kuwa hana chuki na watu pamoja na wasanii wa Tanzania.
“Ndugu zangu wapendwa Tanzania, msije mkadanganyika kufikiria kuwa sipendi nyinyi au wasanii wenu. Sisi sote ni familia, na tunahitaji kila mmoja wetu. Lakini kile sitakachokubaliana nacho ni dhihaka,”aliandika Willy
Hata hivyo kwa upande wa Phina naye hakulikalia kimya akajibu na kuwataka mashabiki kuwekeza nguvu zaidi katika umoja kwenye muziki.
“Tusipoteze mtazamo wetu wa kile kinachotuunganishamuziki. Tusilazimishe muziki kuwa na mipaka kwa sababu muziki hauna mipaka,” aliandika Phina
Wawili hao wameachia ngoma hiyo mapema leo Machi 7, 2025 iitwayo ‘Inabamba’.

Leave a Reply