Muziki wa miondoko ya taratibu Kompa Flava umeripotiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika muziki wa Bongo Fleva huku ukiiteka jamii kutokana na muundo wake wa kipekee.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Audiomack Africa’ umeweka wazi kuwa muundo wa muziki huo umekuwa wa kipekee hasa ukichanganywa na melodi za Kiswahili.
“Kwa kuchanganya melodi za Kiswahili na midundo ya jadi ya ngoma za Haiti pamoja na solo za synth, Kompa Flava imekuwa sauti ya pekee ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2024,” imeandika taarifa kutoka Audiomack Africa
Mbali na kutoa taarifa hiyo lakini pia zipo ngoma ambazo zimepeleke muziki huo kutamba zaidi ikiwemo Zawadi, Pwita ‘Zuchu’, Far Away ‘Genius Jini ft Jay Melody’, ‘Usemi Sina ‘Nandy ft Harmonzie’, Mchuchu ‘Mocco ft Alikiba’, Nisiulizwe ‘Jux’ na nyinginezo.
Kompa Fleva ni aina ya muziki wa taratibu wenye radha ya kipeee ambao asili yake ni Comoro.
Leave a Reply