Moja ya staili ya ushangiliaji ambayo inakubalika zaidi huku ikiwavutia mashabiki wengi ni ambayo amekuwa akiitumia mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Al-Nassr, Cristiano Ronaldo ya kuruka na kisha kurusha mikono.
Inaelezwa kuwa staili hiyo anayotumia CR 7 ameikopi kutoka kwa marehemu mfalme wa Pop Marekani, Michael Jackson ambapo msanii huyo alikuwa akiitumia wakati akitumbuiza kwenye show zake mbalimbali na wakati alipokuwa akifanya mazoezi.
Aidha kwa upande wa Ronaldo alianza kutumia staili yake maarufu ya ushangiliaji, inayojulikana kama ‘Siiii!’ mwishoni mwa miaka ya 2000. Alianza kuitumia baada ya kufunga mabao, hasa akiwa na timu ya Manchester United.
Staili hiyo ilijulikana zaidi baada ya yeye kuhamia Real Madrid mwaka 2009 na kuwa mojawapo ya ishara zinazomfanya kuwa maarufu duniani. Aidha kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa ushangiliaji huo ni kichocheo cha kumfanya mtu kuwa maarufu na mwenye mafanikio zaidi.
Michael Jackson amewahi kutamba na ngoma kama Billie Jean, Thriller, Beat It, Smooth Criminal na nyinginezo, alifariki dunia 25 Juni 2009, akiwa na umri wa miaka 50.
Alifariki kutokana na mshtuko wa moyo uliochochewa na matumizi ya dawa za kupunguza maumivu, hususan propofol, alizokuwa akitumia ili kupata usingizi.

Leave a Reply