Kuruthum Ally : Ubunifu katika biashara utasaidia vijana wengi

Kuruthum Ally : Ubunifu katika biashara utasaidia vijana wengi

Changamoto ya ajira ni kilio cha dunia nzima hususan kwa vijana ambao wengi hujikuta wakizurura mitaani au kuzungunga na vyetu vyao wakisaka ajira ambazo zinazidi kuwa finyu kila uchao.

Sasa kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) iliyotolewa mwaka 2018 dawa mujarabu ya tatizo la ajira kwa vijana ni kujiajiri kwa kutumia fursa zilizopo za mafunzo ya ufundi stadi, teknolojia na ubunifu.

Hapa Tanzania mafunzo ya ufundi stadi yamekuwa mkombozi kwa vijana wengi kama alivyobaini Kuruthum Ally mwanafunzi kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Mikumi Morogoro.

Kuruthum amesomea course ya Secretary and Computer level three na driving course.

Alisema kupitia mafunzo aliyoyapata VETA amefanikiwa kuanzisha biashara ya makeup, kupaka watu ina, kutengeneza kazi mbalimbali za harusi, michango na shughuli nyingine, kupika keki.

Hata hivyo alisema pamoja na ufanyaji wa biashara hizo pia anajishughulisha na uuzaji wa perfyum, pochi za wadada, nguo na mashuka.

Alisema biashara hizo zinamsaidia kujikimu japo biashara ya makeup na ina mara nyingi huwa za msimu tofauti na hizo zingine anazozifanya.

Kuruthum anabainisha kuwa aliamua kufanya biashara hizo kwa sababu ni vitu anavyovipenda hivyo kama ni wazi kuwa lazima utapambana na kuhakikisha unatimiza malengo yako kwa kufanya kile unachopenda.

Changamoto

Alisema amekuwa akikutana na changamoto za kawaida lakini kwa upande wa makeup anakumbana nazo nyingi hasa za kutoaminiwa na wateja kutokana na kutokuwa maarufu.

“Mimi bado sio maarufu katika upande wa Makeup, sasa imekuwa ikichukua muda mtu kuamini kile unachokifanya hasa kama unamfanyia kwa mara ya kwanza, unakuta mteja anakuwa na wasiwasi kama utampamba vizuri, lakini namshukuru Mungu ninapomaliza kumfanyia ujikubali na kusema nimeweza kazi yangu,” alisema

Alisema ipo changamoto nyingine anayokumbana nayo katika upande wa upatikanaji wa material mbalimbali za utengenezaji wa sabuni za maji.

“Kuna wakati material yanakuwa sio makali unakuta sabuni inakuwa maji hata kama vipimo ni vilevile maana sabuni ya maji ukiitengeneza inavyolala ndo inavyokuwa nzito ila material yakiwa sio makali kila ikilala ndo inazidi kuwa nyepesi..

“Changamoto kwenye upande wa kutengeneza kadi huwa ni za kawaida labda mteja kubadilisha ratiba ya shughuli anakuja kukwambia tayari umeshaprinti kazi,” alisema

Faida aliyopata

Alisema moja ya faida aliyoipata kutokana na shughuli anazozifanya kwana kukutana na watu mbali mbali na kubadilishana nao mawazo.

“Kukuwa kimawazo na kujua nini nifanye ama kipi niongeze kwenye biashara ninazofanya pia nimefaidia kupata fedha za kujikimu katika mahitaji yangu muhimu na ya msingi,” alisema

Ushauri wake kwa vijana

Alisema ushauri wake kwa vijana wenzake ni kujishughulisha haijalish amesomea nini huko chuoni.

“Tafuta kitu cha kuongeza katika ujuzi wako ili kupata fedha za kujikimu maana unaweza ukasomea kitu flani ukakosa kuajiliwa  ukiwa na kitu cha ziada kinachokufanya uweze kujiajiri inakuwa ni Jambo zuri na ukawa unajiongezea kipato,” alisema na kuongeza

Pia ata kama umeajiriwa ukiwa na kitu cha ziada nje na ajira yako inakuwa ni jambo zuri na la msingi maana unaweza kujikwamua na maisha yakasonga,” alisema

Hata hivyo Kuruthum alisema ana kitu kingine anachokipenda zaidi ya hivyo anavyofanya kwa sasa anavipenda na kuviheshimu.

Anatamani kuwa ….

Kuruthum anafunguka na kusema anatamani kuwa yeye kama yeye hasa kuongeza kitu flani ili kuweza kufikia ndogo zake alizojiwekea katika biashara zake.

“Natamani kuwa mimi kama mimi, nataka kuwa mkubwa na sitamani kuwa mwingne maana sitafikia ndoto zangu, kiukweli matamanio yangu kuwa nilivyo,” alisema na kuongeza

“Natamani kuwa mimi maana naweza kujielezeaa , mimi mwenyewe naweza kujua nni napenda naweza kufanya lolote, nataka kuwa kama mimi maana ni package iliyojitosheleza na haiitaji nyongeza,” alisema






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags