Lee Jung anawasiwasi kuhusu msimu ujao wa Squid Game

Lee Jung anawasiwasi kuhusu msimu ujao wa Squid Game

Wakati mashabiki kutoka pande zote za dunia wakisubiri kwa hamu toleo la mwisho la filamu ya Squid Game 3. Kwa upande wa Lee Jung-jae anayeigiza kama Seong Gi-hun kwenye filamu hiyo anadai kuwa na wasiwasi namna mashabiki watakavyopokea filamu hiyo.

Baada ya Netflix kutoa trela ya filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Juni 27,2025 Jung-jae aliiambia ‘The Hollywood Reporter’ kuwa wasiwasi wake mkubwa ni mapokezi kutoka kwa mashabiki.

“Tunaenda kutoa hivi karibuni nina wasiwasi sana. Nafahamu kuwa wengi wenu mna hamu ya kujua nini kitaendelea kwenye msimu wa tatu. Lakini sisi sote tunavutiwa zaidi na kujua ni kwa kiasi gani mtafurahia, kwa hiyo siwezi kusubiri nina wasiwasi sana,” amesema Jung-jae

Utakumbuka msimu wa kwanza wa Squid Game ambao uliachiwa rasmi Septemba 17, 2021 uliweka rekodi kushinda tuzo sita za Primetime Emmy, ikiwemo tuzo ya kihistoria kwa mkurugenzi Hwang Dong-hyuk, ambaye alishinda tuzo ya Outstanding Directing kwa Drama Series. Waigizaji Lee Jung-jae na Lee You-mi pia walishinda tuzo kwa ufanisi wao.

Vilevile Netflix iliripoti kuwa ulikuwa ni mfululizo wake maarufu zaidi duniani kwa kipindi hicho, ikifikisha zaidi ya watu milioni 142 wakifungua akaunti kuangalia filamu hiyo pamoja na kupata watazamaji bilioni 2.2 katika wiki yake ya kwanza.

Aidha msimu wa pili wa Squid Game uliachiwa rasmi Desemba 26, 2024 ukinogeshwa na mastaa kama Lee Jung-jae, Lee Byung-hun, Wi Ha-jun, na Gong Yoo. Huku kukiwa na washiriki wapya kama Yim Si-wan, Kang Ha-neul, Park Gyu-young, Lee Jin-uk, Park Sung-hoon, Yang Dong-geun, Kang Ae-sim, Lee David, Choi Seung-hyun, Roh Jae-won, Jo Yu-ri, na Won Ji-an.

Filamu hiyo maarufu ya Kikorea iliripotiwa kuweka rekodi kwa kushika namba moja kwenye nchi zaidi ya 93 ikiwemo Marekani, Honduras, Kenya, Oman, Thailand na nyingine, pia ilifanikiwa kupata watazamaji milioni 68 ndani ya siku nne za kwanza. Rekodi ambayo hapo awali ilishikwa na filamu ya Wednesday, ikipata watazamaji milioni 50.1 katika wiki yake ya kwanza.


Msimu wa kwanza uliingiza zaidi ya dola milioni 900 kwa Netflix, huku ikigharimu takribani dola milioni 21.4 tu kutengenezwa, hata hivyo Squid Game (msimu 1 & 2) umekadiriwa kuingiza zaidi ya dola bilioni 1 kwa Netflix.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags