Magemu bomba   kwa simu za Android

Magemu bomba kwa simu za Android

Kuna magemu mengi sana yanayopatikana playstore lakini leo  tunakuletea orodha ya magemu mazuri kwa simu za android yanayopatikana playstore. Magemu huwa hayabagui umri wala jinsia mtu yeyote anaweza kucheza gemu.

Candy crush saga: Gemu hili lilianzishwa mwaka 2012 na linapatikana kwenye simu za Android, Apple na za Windows. Mpaka sasa gemu hili limepakuliwa Playstore na zaidi ya watu Bilioni 1.

 Gemu hili linapendwa sana na watu kwasababu halichukui nafasi kubwa kwenye simu, ni bure kupakua na pia ni jepesi kucheza. Gemu hili linahusu kulinganisha vitu vitatu na zaidi, yaani mchezaji anatakiwa asogeze kitu kimoja kwenda kukilinganisha na vitu vingine vitatu vinavyofanana nacho.

Temple run: Hili ni gemu linalohusu mchezaji kuchezesha mtu anayekimbizwa na mnyama anayefanana na nyani ambapo mchezaji anatakiwa kukusanya hela na mali zingine akiwa njiani anakimbizwa na mnyama huyo.

Unapokuwa na mali nyingi ulizokusanya unaweza kubadilisha wahusika wa kuchezesha pamoja na kujiongezea uwezo wa wachezaji wako. Gemu hili mpaka sasa limepakuliwa Playstore na watu zaidi ya Milioni 500.

 Pia hili gemu linamuendelezo wake wa Temple Run 2 ambapo mazingira ya gemu yamebadilika lakini uchezaji ni ule ule wa kukimbizwa na mnyama. Kupakua na kutumia gemu hili ni bure.

Asphalt 9 Legends: Hili ni gemu la magari linalohusu mchezaji kuendesha gari na kushiriki mashindano mbalimbali ndani ya gemu hilo. Unaweza kuchagua mazingira na gari ya kutumia katika mashindano hayo.

Gemu hili ni zuri kucheza na pia hukuchangamsha pale unapoboreka. Mpaka sasa gemu hili limepakuliwa na watu zaidi ya Milioni 50 playstore.  

FIFA Football: Hili ni gemu la mpira linalomruhusu mchezaji kucheza mpira kwa kuchezesha wachezaji mbalimbali wa timu aliyochagua kuchezesha. Kuna mambo mengi unayoweza kufanya ndani ya gemu hili kama kununua na kusajili wachezaji, Kuchagua ligi ya kucheza, kuchagua timu ya kuchezesha, uwanja na mengine mengi.

Baadhi ya matumizi ya gemu hili ni ya kulipia lakini kupakuwa gemu hili ni bure. Mpaka sasa watu waliopakua gemu hili playstore ni zaidi ya Milioni 100.

Bus simulator: Hili ni gemu linalohusu mchezaji kuendesha basi kubwa kama madereva wanavyofanya barabarani. Gemu hili linamjengea mchezaji uhalisia uliopo kwa madereva wa mabasi hayo.

 Mchezaji anapocheza gemu hili anapewa maelekezo ya kufanya kama kupaki gari, kuendesha kurudi nyuma. Gemu hili ni bure kupakua na mpaka sasa limeshapakuliwa na watu zaidi ya Milioni 100.

Magemu husaidia kupunguza mawazo na kuchangamsha akili.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags