Maisha hayana formula, USIKARIRI

Maisha hayana formula, USIKARIRI

Mpendwa msomaji wetu leo katika karia tumekusogezea siri ya maisha na kukusisitizia kwamba maisha hayana kanuni lakini yana siri nyingi.

Jongea nasi kuzijua siri hizo……

  1. SIRI YA KWANZA

Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho kinguoni kwako!", Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake!

  1. SIRI YA PILI

Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana?

  1. SIRI YA TATU:

Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja.

  1. SIRI YA NNE

Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matundo ndo unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka!, Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia, ila hujauona.

 

  1. SIRI YA TANO

Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute kama kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?

  1. SIRI YA SITA

Ili ufurahie maisha, jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba!, Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha yako hovyo!

  1. SIRI YA SABA

Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Huyajui ya mama yako kwa sababu baba yako alichagua kuyaficha! Kama unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako.

  1. SIRI YA NANE

Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure. Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende zake, tena mpe na nauli.

  1. SIRI YA TISA

Hata kama umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga. Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike

 

10.SIRI YA KUMI

Haijalishi umri umekwenda kiasi gani kama una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri  ni namba tu na uzee hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags