Mama wa kambo wa Madonna afariki dunia

Mama wa kambo wa Madonna afariki dunia

Mama wa kambo wa mwanamuziki kutoka Marekani Madonna ambaye alimlea kwa muda mrefu aitwaye Joan Ciccone amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Tmz mwanamke huyo alifariki dunia wiki hii baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu.

Joan alikuwa mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo na alitumia muda mwingi kumlea Madonna tangu alipokuwa mdogo, na alifunga ndoa na baba wa Madonn, Silvio Ciccone, miaka michache baada ya kifo cha mama yake Madonna, ambaye pia alifariki kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 30.

Mbali na uhusiano wake wa kifamilia, Joan alionekana katika makala kadhaa za Madonna, zikiwemo “I’m Gonna Tell You A Secret” na kipindi cha televisheni cha “Biography.”

Hata hivvyo mpaka kufikia sasa timu ya Madonna haijatoa taarifa rasmi kuhusu kifo cha Joan, lakini chanzo cha karibu cha msanii huyo kinadai kuwa familia ya Madonna inamkumbuka mwanamke huyo kufuatia na upendo aliyowaonesha enzi za uhai wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags