Mama wa marehemu Carina aeleza magumu aliyopitia mwanaye

Mama wa marehemu Carina aeleza magumu aliyopitia mwanaye

Mama wa aliyekuwa mwigizaji Hawa Hussein ‘Carina’ amesema uvimbe tumboni ndiyo ugonjwa uliomuua mwanaye.

Mama huyo ameiambia Mwananchi kuwa ugonjwa huo umemsumba Hawa kwa miaka nane.

“Mwanangu alikuwa na uvimbe tumboni basi ndio chanzo, akakatwa tumbo hadi kafariki kafanyiwa upasuaji mara 26. Na tatizo likawa linajirudia ndiyo maana zikawa operesheni nyingi.

“Nimebaki na kumbukumbu ya kwamba jana nimeongea naye vizuri sana lakini kumbe sikujua kama anakufa. Ameugua karibia miaka nane ameacha mtoto mmoja anaitwa Aisha,” amesema mama wa marehemu.

Hata hivyo ametoa shukrani kwa Watanzania waliomshika mkono tangu mwanaye alipoanza kuugua.

Utakumbuka Hawa alionekana kama Video Queen kwenye wimbo wa ‘Oyoyo’ wa kwake Bob Junior lakini pia alicheza kwenye tamthilia ya kwanza ya mwigizaji Jacob Stephen ‘JB’ ya mwaka 2017 hadi 2018 iliyoitwa ‘Kiu ya Kisasi’






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags