Man United kuumuza Antony kwa bei ya hasara

Man United kuumuza Antony kwa bei ya hasara

Inadaiwa kuwa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, wapo tayari kumuuza kwa bei ya hasara mchezaji wao #Antony, ikiwa ni miezi 18 tangu mchezaji huyo ajiunge kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 85, akitokea Ajax mwaka 2022.

Winga huyo aliyejiunga na ‘timu’ hiyo kwa pesa nyingi amefanikiwa kufunga mabao nane pekee katika msimu wake wa kwanza, huku akiwa na wakati mgumu nje ya uwanja baada ya kukumbwa na madai ya unyanyasaji dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake, Gabriela Cavallin.

Hata hivyo ‘klabu’ hiyo baada ya kuachana na mchezaji huyo inampango wa kutafuta winga anayeweza kucheza pande zote mbili, pamoja na ‘beki’ wa pembeni, huku wakiwa tayari kusikiliza ‘ofa’ mbalimbali kwa mchezaji wao mwingine #JadonSancho, mwezi Januari.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags