Maneno ya washindi wa BSS 2025

Maneno ya washindi wa BSS 2025


Aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Kusaka Vipaji (BSS) Moses Luka (DRC) ameibuka mshindi katika shindano hilo lililoanza mwishoni mwa 2024 na kumalizika Februari 28,2025.

Moses ambaye ni raia wa Congo amewapiga chini washiriki wengine aliofika nao fainali kama vile Charles Burton (Dar es Salaam),Grace Celestian (Mwanza), Prisca Gretu (Babati),Saluh Kulwa (Dar es Salaam) na Martha May (Uganda).

Akizungumza na Mwananchi baada ya kupata ushindi huo amesema wimbo wa mwisho aliotumbuiza kwenye tamasha hilo ulikuwa maalumu kwa ajili ya nchi yake Congo.

"Muziki ni kila kitu kuhusu Vibe, kuna wakati watu wanataka kuwa katika hali hiyo na wengine hawataki. Mimi wimbo wangu wa mwisho niliimba ulihusu Congo kwa sababu ni nchi yangu na kuna watu wanaendelea kufariki.

"Mimi ni mtu ambaye nafurahia mafanikio ya kila mtu kama mtu anafanya vizuri mimi huwa nampigia makofi, nashangilia. Kwa sababu mwisho Mungu ndiyo anachagua nani mshindi. Mimi ni mtu wa amani kitu kikinitokea ni Mungu alikuwa anajua tangu mwanzo,"amesema

Hata hivyo Saluh Kulwa (Dar es Salaam) aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo, pia alishinda tuzo ya mshiriki maarufu zaidi wa BSS

"Naomba niwaambie tunakwenda kupoteza zile kauli za washindi wa BSS huwa wanapotea. Na hawana mwenendo mzuri. Mimi kwangu mazuri mengi yanakuja. Nashukuru nimepata uzoefu wa watu kutoka sehemu tofauti tofauti, hii ya leo ilikuwa fainali kwa hiyo ilikuwa lazima apatikane mtu mmoja.

"Nimrudishie Mungu shukrani kwa sababu amenipa kibali, mimi nilikuwa tayari kupokea matokeo yoyote hata ya leo. Nimeyapokea na nimefirahi sana. Ninatamani kufanya kazi na wasanii niliotumia ngoma zao na kupata ushirikiano wao,"amesema

Mbali na washindi hao Martha May (Uganda) naye aliibuka mshindi wa tatu BSS 2025. Katika mashindano hayo ya mwaka 2025. Mshindi wa kwanza amejinyakulia kitita cha Sh 20 milioni na safari ya kwenda Afrika Kusini, mshindi wa pili Sh 3 milioni na mshindi wa tatu Sh 1 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags