Mariah Carey huvuna mamilioni ya dola kila mwaka  Krismasi

Mariah Carey huvuna mamilioni ya dola kila mwaka Krismasi


Mwanamuziki kutoka Marekani ambaye amekuwa akitamba na nyimbo za Krismasi Mariah Carey atajwa kuingiza mamilioni ya dola kila mwaka kupitia nyimbo zake hizo.

Carey hupata maokoto hayo kutokana na wimbo wake wa ‘All I Want for Christmas Is You’ huku mwaka 2017 jarida la The Economist likiripoti kuwa mwimbaji huyo alipata dola milioni 60 kutokana na mirahaba ya wimbo huo kati ya mwaka 1994 na 2016, ikiwa ni wastani wa dola milioni 2.6 kwa mwaka.

Wimbo huo unaopendelewa zaidi katika sikukuu za Krismasi ulitolewa kwa mara ya kwanza miaka 30 iliyopita (1994) ukiwa ni moja ya wimbo uliyopo kwenye album aliyoipa jina la ‘Merry Christmas’ ikiwa na nyimbo tisa.

Mwaka 2022, Billboard ilikadiria kuwa Mariah Carey alipata dola milioni 5.3 kutokana na toleo la rekodi kuu la wimbo huo na dola milioni 3.2 kutokana na mirahaba ya uchapishaji, jumla ikiwa ni dola milioni 8.5.

All I Want for Christmas Is You ni wimbo bora zaidi wa Mariah Carey kwa mauzo ya wakati wote. Wimbo huo umeuza zaidi ya nakala milioni 16 na unakadiriwa kuwa umepata dola milioni 100 kutokana na mirahaba kufikia mwaka 2023.
Mbali na hayo pia, ni wimbo wa Krismasi uliopewa mtiririko mwingi zaidi nchini Uingereza, ukiwa na zaidi ya mitiririko milioni 180.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post