Marufuku Miss Kuvaa Wigi

Marufuku Miss Kuvaa Wigi

Waandaaji wa mashindano ya Miss Côte d'Ivoire ‘Ivory Coast’ wameanzisha sera mpya kwa washiriki wa shindano hilo kutotumia nywele za bandia (mawigi) wakati wa shindano.

Sheria hii inakuja ikiwa ni juhudi za kuhamasisha uzuri wa asili na kuthamini nywele za asili za washiriki. Hivyo mshiriki hatoruhusiwa kuongezwa nywele wala kuvaa wigi wakati wa mashindano hayo.

Aidha uamuzi huo unalenga kuongeza hamasa kwa wanawake kujikubali jinsi walivyo huku wanaume wa nchi hiyo wakisisitiza, uzuri wa kweli wa mwanamke unapatikana kupitia nywele zake asili na ndio maana wanawapenda jinsi walivyo.

Sheria hiyo imeanzishwa rasmi mwaka huu (2025) kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya ambapo lengo kubwa likiwa ni kuhamasisha uzuri wa asili.

Mbali na mwaka huu ambao sera hiyo itaanza kutumika rasmi lakini pia katika mashindano hayo ya Miss Côte d'Ivoire mwaka 2023 washiriki walionesha nywele zao za asili kila mmoja.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Februari 15 hadi Machi 10 huku fainali ikifanyika Juni 28, 2025 jijini Abidjan.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags