Matumaini: Nilivimba tumbo, miguu ningefariki baada ya kifo cha Sharobaro

Matumaini: Nilivimba tumbo, miguu ningefariki baada ya kifo cha Sharobaro

Mchekeshaji Matumaini Marthin amesema kama siyo kuokoka kwake angekuwa amefariki dunia tangu mwaka 2013 baada ya kifo cha aliyekuwa mchekeshaji Sharobaro.

Tumaini ambaye miaka ya nyuma alitamba sana akiwa na mwenzake Kiwewe. Kwa sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili. Hata hivyo, ameiambia Mwananchi Scoop kuwa mwaka 2013 aliugua maradhi ya figo ambayo yalimfanya alale kitandani kwa muda mrefu.

"Mimi nimeokoka tangu mwaka 2013, niliokoka nikiwa kitandani kwa maradhi niliyougua. Nilimwambia Mungu kama ikimpendeza kunipa nafasi nyingine ya kuishi nitakutumikia. Kweli nikapona nilikuwa naugua maradhi ya figo ilifeli.

"Nilipona kwa maombi ya watumishi. Hapo ndipo nilijiona nakipawa cha kuimba, lakini kabla nilikuwa sijui kama nitaimba. Nilitoa nyimbo ya kwanza ambayo iliitwa 'Nimepona' nikatoa ushuhuda kwa jinsi nilivyokuwa naumwa nikatoa audio ya pili inaitwa 'Amani ya Bwana,'amesema.

Matumaini amesema alianza kupata maradhi hayo akiwa Msumbiji na kila alipoenda hospitali kufanya vipimo hakuonekana kuwa na tatizo.

"Tulizunguka sana hospitali, mpaka kwenye mji mkuu wa Msumbiji. Lakini tatizo lilikuwa halipo tumbo lilivimba sana na miguu ilivimba. Kila nilipokuwa naenda hospitali nilikuwa sionekani kama nina ugonjwa.

"Lakini baada ya kuvuka sasa, nilienda Muhimbili nako nilichukua vipimo hakuna kilichoonekana baada ya hapo watumishi wakawa wananiombea. Nilikuwa naombewa asubuhi mchana na jioni baada ya wiki, nikachukua tena vipimo iligundulika ni figo imefeli wakasema kuna uwezekano wa kupona nikapewa dawa za miezi mitatu,"amesema

Amesema alipona kwa neema ya Mungu ndiyo maana ameamua kumtumikia. Huku akidai kwa sasa ameandika baadhi ya stori anatarajia kuzicheza hivi karibuni zikiwa na dhima kubwa ya kuelimisha jamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags