Mavazi ya kuvaa wanawake wenye vitambi

Mavazi ya kuvaa wanawake wenye vitambi

Leo katika kapu letu la fashion nimependa nikusogezee kitu ambacho this weekend utajifunza kitu mwanetu, hivi unajua fashion ina bebwa na muonekano sasa ngojea tuongelee mavazi kwatu wenye vitambi.

Kitambi wengi hutafsiri kama mafuta yaliyozidi kuzunguka eneo la tumbo na uweza kutokea kwa watoto, vijana na watu wazima hata wazee wa jinsia zote.

Ni moja ya jambo ambalo huwakosesha sana raha watu wengi haswa wanawake na ndiyo sababu huwapelekea kufanya mambo mbalimbali wanayoamini yatasaidia kukiondoa ikiwemo kufanya mazoezi, diet na njia zinginezo.

Wanawake wengi hulalamika kuwa kutokana na kuwa na kitambi au tumbo kubwa wanashindwa kuvaa mavazi ya aina fulani.
Wanamitindo wengi wanashauri watu wenye vitambi kuvaa nguo ambazo hazitawabana kiasi kwamba mpaka tumbo likaonekana.



Magdalena Singano mkazi wa Chamazi jijini Dar es Salaam anasema huwa anapata wakati mgumu kuchagua nguo ya kuvaa itakayomsaidia kuficha kitambi alichonacho ili awe huru anapokuwa katika mizunguko yake.

“Hii ndiyo moja ya sababu inayonifanya nipambane sana kupunguza uzito niliyonao na kitambi ili niweze kuwa huru kuvaa nguo niitakayo”.
Naye Hafsa Kiswaga mkazi wa Chanika jijini Dar es Salaam anaieleza Mwananchi Scoo kuwa kwa upande wake yeye huvaa nguo yoyote ambayo anajisikia kuvaa kwa siku hiyo bila ya kujali kitambi alichonacho kinaonekana ama la.

“Nikisema nisubiri kitambi kiishe ndiyo nidamshi nitashindwa kuvaa kulingana na wakati mimi ninavaa kile ninachojisikia ikiwa hakiko nje ya maadili” alisema.

Hatukuishia hapo tu kama unavyo jua hili swala limekaa kipana zaidi mfanyabiashara wa nguo za kike katika eneo la Chanika, Warda Rashid anasema kuwa kitambi au tumbo kubwa isiwe sababu ya kumfanya mwanamke kuwa na mawazo na kushindwa kupendeza kwani kuna aina ya mavazi ambayo anaweza kuvaa yakamsaidia kuficha tumbo na bado akapendeza na kuonekana wa kisasa.

Alisema moja kati ya mavazi ambayo huwapendeza watu wenye kitambi au tumbo kubwa ni pamoja na loose dress huku akitoa angalizo kuwa ni vyema isiwe kubwa sana bali iwe inaendana na mwili wa muhusika.

“Loose dress ikiwa kubwa sana inafanya mtu kuonekana mnene zaidi na pengine kusababisha kupunguza ubora wa muonekano wake” alisema.
Pia amesema mavazi yenye peplum (mavazi yasio bana) ni mazuri kwa mtu mwenye umbo na tumbo kuwa kwani husaidia kulificha kutokana na mtindo wake wa kutanuka kidogo kwa mbele na kumfanya kuwa na muonekano wa kawaida.

“Kama una tumbo kubwa na huna vazi la aina hii kwenye kabati lako tunakushauri ukalitafute” aliongezea.

Vilevile amesema ‘sketi’ zenye marinda na inapendeza zaidi ikiwa katika mtindo wa high waist na ikavaliwa juu ya tumbo.

“Pia koti au blazer huwapendeza watu wenye umbo na tumbo kubwa, unaweza kuvaa sketi au suruali ya mtindo wa high waist na ukatupia blazer au koti juu yake”

Aliongezea kuwa sehemu ya msingi ambayo usipozingatia kwa mtu mwenye umbo na tumbo kubwa hata ukivaa nguo nzuri vipi bado isikupe muonekano unaotarajia ni pamoja na nguo za ndani.

Anasema kwa mtu mwenye umbo la aina hiyo kama hatozingatia kuvaa nguo za ndani zinazoendana na umbo lake basi itamfanya tumbo au mwili wake kuonekana mkubwa zaidi.

“Kwa mtu mwenye umbo au tumbo kubwa anapendeza kama atavaa nguo ya ndani ambayo itamsaidia kulibana tumbo lake (chupi au taiti bana tumbo), pia bra nzuri na imara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags