Kama hukuwahi kuona hii, fahamu kupitia Mwananchi Scoop wakazi wa kijiji cha Shirakawa-go, Wilaya ya Gifu nchini Japan wametengeneza mfumo wa kipekee wa kuzuia moto kuunguza nyumba zao.
Kijiji hicho ambacho kimejitenga kabisa na mji wakazi wake wamefunga mashine maalumu za maji ambazo zimewekwa ndani na nje ya nyumba kwa lengo la kujihadhari na majanga ya moto.
Wakati wa janga la moto kutokea baadhi ya wanakijiji ambao wametengwa maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo watakwenda kuwasha pampu za maji zilizofungwa ndani na nje ya nyumba husika ili kuzuia moto usisambae sehemu nyingine.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa inakuja kutokana na wakazi wa eneo hilo kulinda nyumba zao za kihistoria zenye mapaa ya nyasi.
Ili kuhakikisha mifumo hiyo inafanya kazi wanakijiji cha Shirakawa-go hufanya majaribio kwa mwaka mara mbili ambapo siku hiyo huiita ‘Sherehe ya Maji’ pampu za kijiji kizima huwashwa kwa wakati mmoja.
Leave a Reply