Mbwa mmoja kutoka Pennsylvania aitwaye Cecil, amezua gumzo baada ya kutafuna bahasha iliyokuwa na hela $4,000 ambazo mmiliki wake alikuwa ameziweka kwa ajili ya kumlipa mkandarasi kwa kuwawekea uzio.
Inaelezwa kuwa mmiliki wa mbwa huyo aitwaye Clayton Law aliweka bahasha iliyokuwa na $4,000 ambazo ni zaidi ya 10 milioni kwenye kabati lake la jikoni lakini baadaye alimkuta mbwa huyo akiwa anaitafuna huku vipande vingine vya pesa vikiwa vimetawanyika kila mahali.

Leave a Reply