Meya Mexico afunga ndoa na Mamba

Meya Mexico afunga ndoa na Mamba

Meya wa mji mdogo wa Mexico aliefahamika kwa jina la Victor Hugo Sosa, amefunga ndoa na mamba katika tambiko la miaka mingi la mavuno ambapo mchumba wake huyo alitambulika kwa jina la Alicia Adriana

Hugo alionekana akimbusu mnyama huyo, ambaye kinywa chake kulikuwa kimefungwa. Mamba huyo mwenye umri wa miaka saba, aliyepewa jina la utani la 'binti wa mfalme', anadhaniwa kuwakilisha mungu anayehusishwa na ardhi.



Ndoa yake na kiongozi wa eneo hilo inaashiria kuunganishwa kwa binadamu na Mungu. Tamaduni hii inakisiwa ilianzia karne nyingi kwa jamii za kiasili za Chontal na Huave katika jimbo la Oaxaca.

Olivia Perez, mwanamke aliyesimamia kumpamba mamba huyo kwa mavazi ya harusi alisema “Kwetu sisi mamba anawakilisha vitu vingi kwa sababu ni malkia, Binti mfalme analeta maji, mavuno mazuri na mvua”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags