Mfahamu Mwanaume Aliyeishi Uwanja Wa Ndege Miaka 18

Mfahamu Mwanaume Aliyeishi Uwanja Wa Ndege Miaka 18

Mehran Karimi Nasseri, raia kutoka Iran aliwavutia wengi baada ya kuishi katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle, uliopo jijini Paris kwa zaidi ya miaka 18.

Mwaka 1988, Nasseri aliamua kuhamia Uingereza, akisema anataka kuungana na familia yake. Hata hivyo, alipokuwa njiani kuelekea Uingereza, aliripotiwa kupoteza nyaraka zake za uraia. Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle (Paris), hakuweza kuthibitisha uraia wake wala hadhi yake kama mkimbizi, hivyo hakuweza kuruhusiwa kuingia Ufaransa wala kurudishwa Ubelgiji.

Kwa sababu hakuwa na hati halali za kusafiria, mamlaka za uwanja wa ndege zilimzuia kuondoka, na hivyo alianza kuishi katika Terminal 1 ya uwanja wa ndege huo kuanzia 1988 hadi 2006.

Umaarufu na Filamu ya "The Terminal"
Wakati akiwa uwanja wa ndege, Nasseri alifahamika kimataifa kupitia ripoti za vyombo vya habari. Kisa chake kilihamasisha filamu ya "The Terminal" (2004) iliyoongozwa na Steven Spielberg na kuchezwa na Tom Hanks kama mhusika mkuu. Licha ya kujizolea umaarufu lakini pia alifanikiwa kupiga pesa kupitia filamu hiyo.

Umaarufu huo ulimfanya Nasseri kuwa kivutio cha waandishi wa habari kutoka pande mbalimbali za dunia. Kwa muda fulani, alikuwa akifanya mahojiano hadi mara sita kwa siku huku akijipatia jina la "Sir Alfred" na alionekana kufurahia uangalizi aliokuwa akiupata.

Mwaka 1999, alipewa hadhi ya ukimbizi na ruhusa ya kuishi Ufaransa, lakini hakuhamia mara moja. Aliendelea kuishi uwanjani hadi mwaka 2006, alipolazimika kupelekwa hospitalini kwa matibabu kutokana na changamoto za kiafya alizokuwa nazo. Aidha mwaka 2022 baada ya kuwa sawa alirejea Terminal 2F ambapo wiki chache badae alifariki dunia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags