Mfahamu mwanaume aliyepandikizwa mikono

Mfahamu mwanaume aliyepandikizwa mikono


Mwanaume mmoja kutoka nchini India aitwaye Raj Kumar (45) amezua gumzo mitandaoni baada ya madaktari 11 kutoka hospitali ya Sir Ganga Ram kufanikiwa kumpandikiza mikono.

Raj Kumar ambaye alikuwa mchoraji alipata ajali ya treni mwezi Oktoba 2020, ajali ambayo ilipelekea kukatwa mikono, kwa mujibu wa madaktari walieleza kuwa walitumia saa 12 katika upandikizaji wa mikono hiyo.

Mikono hiyo ilipatikana kutoka kwa mwanamama Meena Mehta Makamu mkuu mstaafu wa Shule ya New Greenfield, New Delhi ambaye alieleza kuwa pindi atakapofariki basi viungo vyake apewe mtu mwenye uhitaji.

Kabla ya kifo cha Meena Mehta kutokea mikono yake ilikatwa na kupandikizwa kwa Raj Kumar, na hii iliwezekana kutokana na group lao la damu kuendana. Meena Mehta alifariki 19 Januari 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags