Mfahamu mwanaume mwenye uraibu wa kula mifuko ya plastiki

Mfahamu mwanaume mwenye uraibu wa kula mifuko ya plastiki

Wakati baadhi ya watu wakisumbliwa na uraibu wa vilevi ulevi, sigara na vitu vingine, mfahamu mwanaume mmoja aitwaye Robert mwenye umri wa miaka 32 kutoka Oakland, nchini Marekani ambaye yeye ana uraibu wa kula mifuko ya plastiki.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali inaelezwa kuwa Robert alianza kula mifuko hiyo tangu akiwa na umri wa miaka saba na hadi kufikia sasa amekula mifuko zaidi ya elfu 60,000.

Katika kuhakikisha anatimiza haja yake kuna muda anadiriki hadi kuiba mifuko kwenye Super market anapokwenda kununua bidhaa.

Mifuko hii huila kama chakula ambapo huanzia asubuhi na hupendelea zaidi kula mifuko yenye rangi ya bluu. Licha ya ukweli kwamba ulaji wa mifuko unaweza kusababisha madhara kwenye mapafu, lakini kwake aliwahi kufanyiwa vipimo na hakukutwa na tatizo lolote.

Mwanaume huyo ameoa na kwenye ndoa yake alishindwa kula keki iliyoandaliwa kwa sababu tayari alikuwa amekula mifuko mingi kwa siku hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags