Mjukuu wa Mfalme kutoka Dubai, Sheikh Hamdan Bin Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, aliwahi kuwavutia watu wengi huku akipokea pongeze kede kede baada ya kuacha kutumia gari yake aina ya Mercedes-AMG G63 SUV kwa sababu ya kiota cha ndege.
Inaelezwa kuwa Hamdan aliacha kuendesha gari hilo ili kupisha ndege ambaye alikuwa akitengeneza kiota kwa ajili ya watoto huku akiwakataza wafanyakazi wake wa nyumbani kutokaribia gari hilo kuepusha usumbufu kwa ndege huyo.
Aidha mbali na hilo ili kuonesha msisitizo zaidi aliamua kulizungushia gari yake utepe wa tahadhari wenye rangi nyeupe na nyekundu kwa lengo la kuwatahadhalisha watu wengine waokuja nyumban kwake.
Video hiyo ilisambaa kwa kasi, ikikusanya watazamaji milioni 1.5 ndani ya saa chini ya 24 huku mpaka kufikia sasa ikiwa na zaidi ya watazamaji 3.6 kupitia mtandao wa Instagram.
Leave a Reply