Mke wa Mohbad akanusha kupima DNA kwa  siri

Mke wa Mohbad akanusha kupima DNA kwa siri

Omowunmi Aloba, maarufu Wunmi mke wa marehemu msanii kutoka nchini Nigeria Mohbad amekanusha kufanya vipimo vya siri vya nasaba deoxyribonucleic acid (DNA) kwa mwanaye, Liam Mohbad.

Hii ni baada ya kuzuka kwa uvumi kupitia mitandao ya kijamii ikiripoti kuwa wakati baba mkwe Joseph Aloba (baba mzazi wa Mohbad) akisisitiza uchunguzi wa DNA ufanyike dhidi ya mjukuu wake Liam, Wunmi alifanya vipimo vya siri ndiyo maana hataki kutoa majibu.

Kwa mujibu wa chombo cha haabari cha ‘Sahara Reporters’ kilidai kuwa waliwasiliana na Wunmi siku ya jana Alhamisi Mei 2, 2024 kujua kwa undani kuhusu uvumi huo ndipo mwanadada huyo aliweka wazi na kueleza kuwa hakuna ukweli wowote kwenye hilo.

Tangu kifo cha Mohbad, kumekuwa na mzozo kuhusu baba wa Liam, huku baadhi ya wananchi na baba Mohbad wakiomba uchunguzi wa DNA ufanyike kwa Liam, ambapo mwanadada huyo alieleza kuwa inabidi baba Mohbad apate ruhusa kutoka Mahakamani ili aweze kumuachia mwanaye kupima DNA.

Mohbad alifariki Septemba 12, 2023 jijini Lagos akiwa na umri wa miaka 27 huku uchunguzi wa kifo chake bado ukiwa unaendelea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags