Mlinzi wa shule apigwa risasi ya kichogo akiamulia ugomvi

Mlinzi wa shule apigwa risasi ya kichogo akiamulia ugomvi

Mlinzi wa shule ya Thomas R. Proctor, iliyopo New York apigwa risasi kichogoni wakati akizuia ugomvi, katika eneo la kuegesha magari lililopo karibu na uwanja wa mpira wa shule hiyo.

Inaelezwa kuwa kulikuwa na tukio la mashindano ya mpira wa miguu shuleni hapo ndipo nje ya uwanja katika eneo la kuegesha magari ulizuka ugomvi ambao haukueleweka chanzo chake ni nini, mara baada ya mlinzi huyo kusogea ili kuzuia ugomvi alijikua akifyatuliwa risasi kichwani katika eneo la kichogo.

Baada ya tukio hilo mlinzi huyo alifanikiwa kukimbizwa hospitali akiwa kwenye hali mbaya kwa ajili ya kupata matibabu, na hadi sasa bado hali yake haijaimarika yupo chini ya uangalizi wa madaktari.

Hata hivyo Polisi wanaendelea kumsaka mshambuliaji huku shughuli za shule hiyo zikiwa zimeghairishwa, kwa ajili ya kutoa huduma ya msaada wa  afya ya akili kwa wanafunzi ili kuwatoa kwenye wasiwasi, kutokana na tukio hilo, la kigaidi lililotokea.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags