Msanii Prezzo atangaza kugombea urais Kenya 2027

Msanii Prezzo atangaza kugombea urais Kenya 2027

Msanii wa rap kutokea nchini Kenya, Prezzo ameendelea kuweka wazi nia yake ya kuingia kwenye siasa na kugombe nafasi ya Urais kupitia chama chake cha 'CMB' ( Chama Mabadiliko Busara) katika uchaguzi mkuu utakao fanyika 2027 nchini humo.

Prezzo amethibitisha hilo kwenye mahojiano yake aliyofanya hivi karibuni akisema mipango aliyonayo juu ya chama hicho na dhumuni lake kwa wa Kenya.

"kitu ambacho naweza kukwambia sasa hii ni jina la chama changu ambalo ni Chama Mabadiliko Busara ambacho kitakuwa kila mahali," amesema Prezzo.

Prezzo amesema chama hicho kimelenga zaidi kuleta mabadiliko akiungana na vijana wa Gen Z ambao tayari wameshaonesha kuukataa ukabila.

"Gen Z wametuonesha kwamba wamevunja ukabila hawana ukabila kabisa," amesema

Pia, amesema kuwa alama itakayotambulisha chama hicho ni mikono iliyoachanishwa kutoka kwenye minyororo au pingu.

"Ishara ya chama ni mikono miwili ambayo mnyororo au pingu imekatika kuonesha" amesema.

Hata hivyo, kauli yake imeibua maoni mengi kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakihitaji kumuona namna atakavyotoa hotuba zake wakati wa kuomba kura.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags