Mtoto wa Diddy ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono

Mtoto wa Diddy ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono


Mtoto wa Diddy, aitwaye King Combs (26) ameshtakiwa kwa kumnyanyasa kingono mwanamke aliyefahamika kwa jina la Grace O'Marcaigh, tukio lililotokea St Martin mwaka 2022.

Kwa mujibu wa Tmz, Grace ambaye ni muhudumu ya boti amedai kuwa tukio hilo lilitokea kwenye Yatch wakati wa likizo ya familia ambapo King alimlazimisha kufanya naye mapenzi bila idhini yake huku akiweka wazi kuwa kuna ushahidi wa video pamoja na sauti.

Hata hivyo kwa mujibu wa nyaraka zilizofikishwa mahakamani zinaeleza kuwa Diddy amejumuishwa katika kesi hiyo kutokana na kulikalia kimya suala hilo toka mwaka 2022.

Aidha wakili wa Diddy na King, Aaron Dyer, alidai kuwa kesi hiyo haina ukweli wowote hivyo anaanda nyaraka za ombi la kufuta kesi hiyo mahakamani.

Ikumbukwe kuwa #KingCombs amewahi kuhusishwa kuwa kwenye mahusiano na wanawake tofauti tofauti akiwemo #BreaHick ambaye alidumu naye kwa miaka kadhaa na sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo #RavenTracy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags