Mtoto wa Gaddafi yuko mahututi

Mtoto wa Gaddafi yuko mahututi

Mmoja wa watoto wa kiume wa marehemu kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, Hannibal Gaddafi ameripotiwa kuhamishwa kutoka jela ya Lebanon, ambako amekuwa kwenye mgomo wa kula, na kupelekwa hospitali akiwa katika hali mbaya.

Shirika la habari la Reuters linanukuu Televisheni ya Al-Hadath likiripoti kwamba kiwango chake cha sukari kwenye damu kilishuka sana.

Hannibal Gaddafi amekuwa gerezani nchini humo kwa zaidi ya miaka minane. Aligoma kula mwezi uliopita akipinga kuzuiliwa kwake kwa muda mrefu bila kufunguliwa mashtaka.

Ikumbukwe tu Hannibal amekuwa akishikiliwa tangu alipokamatwa nchini Syria alikokuwa amekimbilia baada ya kuuawa kwa babake na waasi mwaka 2011.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags