Duane “Keffe D” Davis ambaye ni mwanachama wa zawani wa genge la ‘Southside Compton Crips’ kutoka California, Marekani anayetuhumiwa kwa mauaji ya Tupac Shakur, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi Septemba 7, 1996, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu afikishwe gerezani.
Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘ABC News’, Duane amezungumza kutoka gerezani kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mwaka 2023 anadai kuwa hana hatia yoyote na anapaswa kuwa nyumbani akifurahia maisha na familia.
“Ninapaswa kuwa huko nje nikifurahia maisha yangu ya uzeeni katika moja ya mechi za mpira wa miguu au mpira wa kikapu za mjukuu wangu. Nikifurahia maisha na watoto wangu.
Mimi ni msafi. Sijamuua mtu yeyote ninajuta sana, kujadili hadharani kifo cha Shakur kwa sababu za kifedha, wamenishikilia tu na hawana ushahidi wowote hawana bunduki, gari, wala ushahidi wowote ule unaothibitisha kufanya mauaji hayo,” amesema Keffe D
Hata hivyo, waendesha mashtaka wa Nevada wanadai kuwa Davis, alikuwa kiongozi wa kundi lililomuua Shakur huku mtuhumiwa huyo akikana mashitaka ambapo wakili wake anajaribu kufuta kesi hiyo akidai kuwa mteja wake hakupaswa kushtakiwa kwani hana hatia. Kesi yake imepangwa kuanza kusikilizwa Februari 9, 2026.
Tupac Shakur alizaliwa Juni 16, 1971, na alifariki Septemba 13, 1996 baada ya kupigwa risasi Septemba 7, 1996, huko Las Vegas, Nevada.

Leave a Reply