Mwakinyo kuingia ulingoni Zanzibar

Mwakinyo kuingia ulingoni Zanzibar

Licha ya kufungiwa mwaka mmoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania Bara (TPBRC), bondia Hassan Mwakinyo ameibukia visiwani Zanzibar na anatarajiwa kuingia ulingoni Novemba 24, katika pambano la kimataifa.

Kwa mujibu wa #Mwanaspoti imeeleza kuwa mmoja wa kiongozi wa Kamisheni ya ngumi za Kulipwa #Zanzibar imelithibitishia gazeti hilo kwa kusema kuwa

“Ni kweli #Mwakinyo aliomba kuwa bondia wa huku na kuna pambano anatakiwa apigane Novemba 24 pale Ngome kongwe.

Pambano lipo, kinacho chelewesha kutangazwa ni kesi yake ya Bara ambayo waziri wa michezo wa huku aliagiza baraza la huku liifuatilie kujua nini kinaendelea ndipo litangazwe” amesema mmoja wa viongozi wa juu wa kamisheni hiyo na aliomba jina lake lisitajwe

Aidha Katibu mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha ametafutwa kwenye simu amesema

“Lipo Novemba 24, lakini tunasubiri maelekezo kutoka kwa wenzetu wa BMT, ninacho kifahamu ni Mwakinyo alifungua kesi kupinga adhabu aliyopewa na TPBRC na juzi ndiyo ilisikilizwa na baraza la Bara.

Kwa upande wa bondia Mwakinyo alipotafutwa juzi na jana simu yake haikupokelewa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags