Namna ya kurudisha hisia za mapenzi zilizo potea

Namna ya kurudisha hisia za mapenzi zilizo potea

Hellow! Haya kama kawaida yetu kuwaletea vitu konki kuhusiana na maswala mazima ya ndoa na mahusiano, sasa leo tumekuja kuzungumza na nyie kuhusiana na tatizo ambalo wanakumbana nalo baadhi ya watu la kukisa hisia wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Tunaishi kwenye ulimwengu unaoenda kasi sana kiasi kwamba usipokuwa makini, unaweza kujikuta ukimpoteza mtu uliyempenda sana maishani kwa sababu tu ya kutojua namna ya kwenda naye sawa.

Inafahamika kwamba mapenzi ni hisia lakini ni wachache wanaoweza kueleza jinsi ya kufanya hisia za mapenzi ziendelee kuwa hai. Siku hizi ndoa nyingi zinaendelea kuwepo kwa sababu ya kudra tu, unakuta mume na mke wanaishi kwa sababu ya mazoea tu lakini si kwa sababu ya mapenzi!

Wengine wanakwambia kabisa mapenzi yalikuwa wakati tunaanza mahusiano lakini sasa Wanaishi tu ilimradi siku zinaenda, ilimradi wanawalea watoto lakini si kwa sababu ya upendo kati yao.


Wengine wanafikia hatua hata ya kulala mzungu wa nne au kutengana vyumba kabisa! Au kwenda kulala vyumba vya watoto, watu haohao Kwa nje mnawaona kama wanapendana lakini kumbe ndani kuna ufa mkubwa kati yao, hakuna tena mapenzi kati yao.

1. Weka mazoea ya kurudi mapema nyumbani, na kupunguza ubize ukiwa nyumbani usiwe na mambo ya kuhamisha ofisi nyumbani, badilisha utaratibu, anza kutenga muda wa kutosha wa kukaa naye karibu na kuwa mnyenyekevu kwake.

Siyo unawahi kurudi nyumbani halafu muda wote mna kazi ya kubishana na kulumbana! Jifanye mjinga, jishushe na muoneshe kwamba unampenda! Hata kama alikuwa na dukuduku lake moyoni, litaanza kupungua, ataanza kuzungumza na wewe, ataanza kukuchangamkia na hapo utakuwa umefanikiwa kuanza safari ya kuziamsha upya hisia zake.

2. Tafuta muda wa kutoka naye ‘out’, mpeleke maeneo mliyozoea kwenda kipindi mapenzi yenu yalipokuwa motomoto, taratibu hisia zitakuwa zinaendelea kuongezeka kidogokidogo, jamani wewe toka ulivyo muoa mtoto wa mama mkwe yupo tu hajawahi kutolewa out kwenda hata sehemu nzuri.

 3. Mtunze Mume\ Mke wako, Hisia za mapenzi ni kama bustani ya maua, haiwezi kustawi wala maua hayawezi kuchanua na kutoa harufu nzuri kama huitunzi bustani yako kila siku, Hisia za mapenzi siyo kitu cha kuja na kupita, unatakiwa ushughulike na hisia za mwenzi wako kila siku.


unachotakiwa kukifanya, unapoona unaishi kwenye maisha ambayo hisia za mapenzi kati yako na mwenzi wako hazipo tena, ni kuanza kujiweka karibu na mwenzi wako, kimletea zawadi kila utokapo, kumtafuta mara kwa mara ukiwa mbali nae

i hope kuna kitu umejifunza mtu wangu wa nguvu, endelea kupitia page yetu ili uweze kujifunza mambo mengi zaidi kama unavyo jua hatunaga mba mba mba.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags