Namna Ya Kutengeneza Juisi Ya Viazi Vyekundu (Beetroot)

Namna Ya Kutengeneza Juisi Ya Viazi Vyekundu (Beetroot)

Juisi ya beetroot ni nzuri kwa moyo wako ikiwa na faida zaidi ya moja. Antioxidants, vitamini, na madini katika juisi ya beet husaidia kupunguza uvimbe, kuboresha mzunguko wa damu, na kuzuia mkazo wa oksidi, ambayo yote ni ya manufaa kwa afya ya moyo.

Tunda hilo lina Vitamini: A, C, na B-tata, madini: Potasiamu, chuma, magnesiamu na manganese, Antioxidants: Betalains, ambayo hutoa beets rangi nyekundu, Nitrati: Michanganyiko inayobadilika kuwa nitriki oksidi mwilini. 

Wakati baadhi ya watu wakiamini kuwa juisi hiyo hunywewa hasa na wanawake wenye ujauzito kwa ajili ya kuongeza damu, basi nipo hapa kutengua kauli hiyo kwani juisi inayotengenezwa na tunda la Beetroot (Viazi vyekundu) si lazima inywewe na wajawazito hivyo mtu yeyote anaweza kutengeneza kwa ajili ya familia ama biashara. 

Na kama unataka kujua namna ya kutengeneza juisi hii basi ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kwa ajili ya dondoo zaidi…

 

MAHITAJI

1.Beetroot (viazi vyekundu) 3-5)

2.Malimao makubwa mawili.

3.Asali vijiko viwili vikubwa.

4.Tangawizi au hiriki (sio lazima sana kuweka).

5.Maji nusu lita (hapa inategemea na juisi yako unataka iwe na uzito kiasi gani, ukiweka maji mengi itakuwa nyepesi.

 

Mbali na tunda hilo kutengenezwa pekee kwa ajili ya kuimarisha afya lakini pia unaweza kulichanganya tunda hilo na matunda mengine kama vile embe, karoti, apple na mengineyo kutengenezea juisi.

 

NAMNA YA KUTENGENEZA

Hatua ya kwanza: chukua viazi vyako na uanze kuvimenya vyote, baada ya hapo vikate kisha viweke kwenye bakuli kubwa.

 Hatua ya pili: baada ya hapo chukua tangawizi yako ikatie katika bakuli ulilowekea viazi vyako na ukishamaliza hapo tia kwenye brenda na uanze kuisaga. 

Hatua ya tatu: ukishamaliza kuisaga kunachofuata ni kuichuja, ukishamaliza kuichuja sasa hapo unaweza kutia asali yako, maji ya limao pamoja na hiriki. 

Mpaka kufikia hapo juisi yako yenye mchanganyiko wa vitu vitatu viazi, limao na asali itakuwa tayari kwa ajili ya kunywa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags