Ndumbaro mgeni rasmi Gland Gala Dance

Ndumbaro mgeni rasmi Gland Gala Dance

Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Gland Gala Dance litakalofanyika Superdome Masaki jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Chocolate Princes, Mboni Masimba ambaye ndiye mwandaaji wa tamasha hilo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Masimba amesema tamasha hilo litafanyika Agosti 30, mwaka huu ambapo miongoni mwa bendi zitakazotumbuiza ni FM Academia, Twanga Pepeta, Tukuyu Sound na Malaika Band.

Kwa upande wake Pacho Mwamba ameomba watu wengi kujitokeza kwenye tamasha hilo wakiwemo wanamuziki wa Tanzania ili wajifunze mengi ikiwemo namna ya kuimba "live".

Charz Baba naye amesema: "Siku hiyo ya tamasha, Twanga Pepeta tutaingia ukumbini  tukiwa na ubunifu mpya, nyimbo zetu za zamani na mpya tutaziimba siku hiyo."

Christian Bella kwa upande wake amesema: "Nitaanza kufanya mazoezi mapema kwa ajili ya kutoa burudani nzuri siku hiyo, nawaahidi sitawaangusha mashabiki wa muziki wa dansi, waje tu kwa wingi."

Ikumbukwe kuwa Gland Gala ilianza mwaka 2022 kwa lengo la kutoa burudani ya Muziki wa Dansi na kuupa thamani muziki huo, kwa mara ya kwanza mgeni rasmi alikuwa mwanasiasa mkongwe Abdulrahman Kinana, na mwaka jana lilifanyika Mbeya, mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post