Niffer kuanzisha timu ya mpira wa miguu kwa Wanawake

Niffer kuanzisha timu ya mpira wa miguu kwa Wanawake

Watu weweeee kitaa kimeitikaa leta mpira tupige mbugi na kumpiga teke chura ni sawa na kumuongezea mwendo,wacha maneno weka vitendo maneno ya waswahili hayo baada ya mwandada Niffer kuibuka na kuanzisha timu ya mpira wa miguu kwa wanawake.

Mwanadada huyo ambaye wengi tumefahamu kupitia biashara yake ya uuzaji vipodozi na nguo na wengine  wakamfahamu baada ya kuhusishwa kwenye ugomvi na staa wa muziki Gigy money.

Niffer kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe huu hapa

“It has always been my dream,nilishasema mimi nikishindwa kucheza,basi wasichana wenzangu wenye vipaji vya kucheza mpira watacheza”



Pia akaendelea kuandika “I have big visions for this thing, kwa sasa naweza nisieleweke ,but TRUST me! We are going to be game changers! It might not be this soon! But we surely gonna be something else,Football has a place in my heart! And yeah wait and see”

Mwadada huyo akamalizia kuandika “Girls,huu ni wakati wa sisi kuzipambania haswa ndoto zetu na nitafanya kuwainua wenzangu kila ninapo pata nafasi”

Haya wapenzi wa mpira hiyo ni nafasi kwenu kuonyesha uwezo wenu na siye wapenzi watazamaji tuko tayari kabisa kushangilia mbugi la watoto wa kike katika kukuza tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags