Umewahi kufikiria kununua kilo ya nyama kwa laki nane? kama jibu ni hapana fahamu kuwa kuna baadhi ya nchi watu hununua kwa bei hiyo.
Nchini Japan hutumia gharama hiyo kununua kilo ya nyama ya ng’ombe aina ya Wagyu ambae huuzwa kwa dola 350 ikiwa ni zaidi ya Sh 889,000 huku kwa ng’ombe mzima akiuzwa dola 30,000.
Kwa nini nyama ya Wagyu ni ghali sana?
Nyama hiyo huwa na gharama zaidi kutokana na ng’ombe wake kula chakula maalumu chenye protini na asidi ya mafuta ya omega, lakini pia ng’ombe hao huishi katika mazingira tofauti na wanyama wengine. Hivyo hata mazingira ya ukuaji ni tofauti na ng'ombe wengine.
Mbali na hayo nyama ya ng’ombe wa Wagyu huwa na ladha ya kipekee kama vile ya siagi ambayo inawafanya watu kuipendelea zaidi na kukubaliana na gharama hiyo.
Mbali na nyama hiyo kuwa ghali zaidi ulimwenguni nyama nyingine ambayo inadaiwa kuwa ghali zaidi ni ng’ombe aina ya Kobe ambayo ni nadra sana kupatikana.
Leave a Reply