OMMY DIMPOZ: Hakuna aliyesomea maisha

OMMY DIMPOZ: Hakuna aliyesomea maisha

Ebwana moja kati ya ujumbe ambao ameutoa msanii wa bongo fleva Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' baada ya kuanza mwaka mpya 2022 ambapo anasema watu wasikate  tamaa kwani hakuna aliyesomea maisha cha msingi ni kupambana, kuwa na nidhamu na juhudi ili kufikia ndoto zao.

Ujumbe huo ameandika kwenye page yake ya Instagram unaeleza kuwa "Cha muhimu ni kupambania ndoto zetu na kuwa focused hakuna aliyesomea maisha, ukiwa na nidhamu na juhudi huku ukimuomba Mungu basi jua wakati wako utafika na riziki yako itaongezeka wala tusioneane choyo pale mwenzako anapopiga hatua".

"Tusikate tamaa wala kuhuzunika pale unapopata vikwazo kwenye utafutaji wetu kwani hata mitume ilipigwa vita na kuchukiwa itakuwa wewe mtoto wa Binti Saidi".

 

Yap huo ndiyo ujumbe alioutoa Ommy Dimpoz bwana, unaweza dondosha comment yako hapo chini ukachangia alichokizungumza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags