‘The God Son’ ya Marioo inatarajiwa kutoka hivi karibuni ikiwa na nyimbo 17 huku wasanii mbalimbali akiwemo Alikiba, Harmonize, Kenny Sol, Aslay, Joshua Baraka wakiwa wamesikika

Marioo alitangaza ujio wa albumu hiyo mpya mapema mwaka huu huku akisisitiza kuwa na nyimbo zenye sound tofauti na iliyozoeleka Bongo.
Hii itakuwa album ya pili kwa msanii huyo kwani mwaka 2022 aliachia album aliyoipa jina la ‘The Kid You Know’ iliyokuwa na nyimbo 21.
Album hiyo imependezeshwa na ngoma kama Allhamdulillah, Why, Hakuna Matata, 2025, Wangu, Salio, Unanichekesha na nyinginezo.
Leave a Reply