Pedi kutolewa bure, Scotland

Pedi kutolewa bure, Scotland

Scotland itakuwa Nchi ya kwanza duniani kuanzisha sheria ya kulinda haki ya bidhaa za hedhi na kutolewa bure nchini humo ambapo leo jumatatu sheria ya bidhaa za kipindi itakapoanza kutumika, Mabaraza na Watu wanaotoa huduma ya elimu nchini Scotland watahitajika kisheria kuhakikisha kuwa bidhaa za usafi zinapatikana kwa yeyote anayezihitaji bila malipo yoyote.

Kwa sasa bidhaa kama vile taulo za kike zinafadhiliwa na Serikali na hupatikana bure katika shule, vyuo na vyuo vikuu nchini Scotland.

Tangu 2017 karibu pound milioni 27 zimetumika kutoa ufikiaji katika mipangilio ya umma ambapo Katibu wa Haki za kijamii Shona Robison alisema kutoa bure bidhaa za usafi kwa Mtoto wa kike katika siku zake za hedhi ni msingi wa usawa na utu na huondoa vikwazo vya kifedha ili kuzipata"

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags