Penzi La Jamie Foxx Na Alyce Huckstepp Lafikia Mwisho

Penzi La Jamie Foxx Na Alyce Huckstepp Lafikia Mwisho

Mwigizaji na mchekeshaji kutoka Marekani Jamie Fox ameripotiwa kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Alyce Huckstepp baada ya kudumu kwa mwaka mmoja kwenye uhusiano wao.

Kwa mujibu wa tovuti ya People chanzo cha karibu cha mwigizaji huyo kiliiambia tovuti hiyo kuwa wawili hao hawapo tena pamoja huku Foxx akioneka kuwa na furaha zaidi kwa wakati huu.

“Jamie yuko bize sana, na anapenda hivyo, Ana mambo mengi sana yanaendelea hadi hana muda wa kusimama na kutafakari jinsi ya kusuruhisha uhusiano huo, yupo tu Ameendelea kufurahia maisha,” kimeeleza chanzo hicho.

Foxx na Huckstepp walitangaza uhusiano wao na kuchumbiana Agosti 2023 kwenye moja ya mgahawa uliopo Malibu, California. Mwigizaji huyo amekuwa kwenye mahusiano na wanawake mbalimbali huku wengine akipata nao watoto akiwemo Connie Kline, Kristin Grannis na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags