Professor Jay Atoa Ushuhuda Maumivu Ya Ugonjwa Wa Figo

Professor Jay Atoa Ushuhuda Maumivu Ya Ugonjwa Wa Figo

Mwanzilishi wa Taasisi ya Professor Jay (Professor Jay Foundatison), Joseph Haule akitoa ushuhuda wake kuhusu ugonjwa wa figo uliomsumbua kwa muda mrefu.

Ushuhuda huo aliutoa baada ya wataalamu wa magonjwa yasio ambukiza kutoa elimu katika hafla iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu magonjwa hayo, jijini Dar es Salaam.

Utakumbuka Profesa aliugua kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu huku akifichua sababu ya ugonjwa wake kupitia wimbo wake wa Siku 462 aliomshirikisha Walter Chilambo kwa kudai kwamba katika kipindi chote alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo.

Mbali na kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii pia Professor Jay ni mwanamuziki ambaye amewahi kutamba na ngoma kama Zali la Mentali, Kamili Gado, Utanambia nini, Kikao cha Dharura na nyinginezo.


Picha naMichael Matemanga






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags