Raia waandamana kutaka afisa polisi akamatwe

Raia waandamana kutaka afisa polisi akamatwe

Maelfu ya watu nchini Ufaransa wameandamana kwenye kitongoji cha kifahari cha Paris Nanterre siku mbili baada ya Afisa wa Polisi kumpiga risasi Nahel M, kijana mwenye umri wa miaka 17 kwenye kituo cha barabara.

Waandamanaji hao wakiongozwa na mama wa kijana huyo walisikika wakisema “Haki kwa Nahel”, baadhi wakiwa na mabango yalioandikwa kwamba, “Polisi wanaua”, wakati wa maandamano hayo yaliyoanza kwa amani lakini yakamalizika kwa ghasia.

Licha ya Afisa wa Polisi huyo aliyempiga risasi Nahel kufunguliwa mashitaka ya mauaji na kisha kushikiliwa kwenye kizuizi cha muda lakini wakili wake ameambia moja ya chombo cha habari nchini humo kwamba afisa huyo hakuwa amevunja sheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags